EWURA YAKUSANYA MAONI YA WANANCHI JUU YA BEI ZA UMEME ZINAZOPENDEKEZWA KIJIJI CHA MALANGALI, WILAYA YA KILOSA, MOROGORO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 22, 2022

EWURA YAKUSANYA MAONI YA WANANCHI JUU YA BEI ZA UMEME ZINAZOPENDEKEZWA KIJIJI CHA MALANGALI, WILAYA YA KILOSA, MOROGORO


Na Mwandishi wetu - Kilosa 

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo Tar.22/08/2022,imefanya mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi juu ya bei mpya za umeme zilizopendekezwa na kampuni inayozalisha umemejua ya Husk Power System Ltd, na kusambaza kwa wananchi wa kijiji cha Malangali, Wilaya ya Kilosa,mkoa wa Morogoro.

Akitoa maelezo mafupi ya ufunguzi wa mkutano huo, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Ambaye ni Afisa Mkuu Huduma kwa Wateja Bw. Michael Mshigwa, amesema EWURA imeendelea kutekeleza agizo la Serikali kwa kuwataka wazalishaji wa umeme wadogowadogo kuwasilisha gharama zao EWURA ili zifanyiwe tathimini ya kina kwa kuzingatia maoni ya wadau na kuwezesha Bodi ya EWURA kuidhinisha bei kwa mujibu wa sheria.

Aidha, mgeni rasmi katika mkutano huo, aliyeshiriki kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilosa Bw. Yohana Michael Kasitila aliwataka wananchi kutoa maoni bila kusita, kwani maoni yao ndiyo yatapelekea wao kupata huduma bora na kwa gharama nafuu.

Wakitoa maoni yao, wananchi wa kijiji cha Malangali wamemtaka mtoa huduma kuhakikisha ubora na uhakika wa huduma ya umeme na kwamba bei yoyote itakayopangwa wao wapo tayari kulipa, na wengine kutaka hata iwe shilingi elfu tano kwa mwezi mradi tu huduma ipatikane.

Wadau wengine waliotoa maoni ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali la EWURA (GCC) na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za EWURA (EWURA CCC)

EWURA inalo julumu la kuhakikisha huduma za umeme, petroli,gesi asilia, na maji na usafi wa mazingira zinapatikana katika ubora stahiki na kwa gharama halisi.

No comments:

Post a Comment