Na Mwandishi wetu Arusha
Katika kuhakikisha zoezi la usajili wa wakulima linakwenda na muda, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania(TFRA), Kanda ya Kaskazini, Gothard Liampawe amekutana na kufanya majadiliano na wataalam kutoka mtandao wa simu wa Airtel na kupanga namna zoezi hili litakavyoendeshwa.
Majadiliano hayo yamefanyika katika ofisi za TFRA kanda ya Kaskazini leo tarehe 5 Oktoba, 2022 ambapo wamekubaliana kuanza zoezi hilo mapema wiki kesho.
Kaimu Meneja Liampawe aliwashauri wataalam hao kutoka Airtel kusajili wakulima bila kujali endapo wanatumia mtandao wa airtel kwenye mawasiliano yao.
Awali ya yote wamekubaliana kuanza usajili kwa wakulima waliosajiliwa kwenye daftari zilizosambazwa kwenye ofisi za halmashauri hizo na baadaye watajiunga kusajili wakulima watakaokuwa wakiendelea kusajiliwa kwenye vitabu katika ofisi za vijiji na vitongoji.
Juhudi hizi ni jitihada za serikali kuhakikisha mkakati wa kusajili wakulima kwenye mfumo wa kidigitali linakamilika na kuwawezesha wakulima kunufaika na mbolea za ruzuku zinazotolewa na serikali ya awamu ya sita.
No comments:
Post a Comment