Na Okuly Julius-Dodoma
IKIWA ni siku moja kupita tangu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, umoja wa wanawake Tanzania UWT kimempongeza Dkt Samia suluhu hassan kwani ni mwenyekiti wa kwanza Mwanamke Tangu Chama cha mapinduzi kianzishwe mwaka 1977.
Akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Mwenyekiti wa umoja wa Wanawake Taifa Marry Chatanda amesema baadhi ya wanachama na viongozi mbalimbali wamemtaja Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuwa ni mmoja wa wanamke shujaa wanaotambuliwa kimataifa kwa utendaji kazi wake wa vitendo.
Aidha, Marry chatanda amewasisitiza wanachana hao kuwa wamoja na kuvunja makundi waliokuwa nayo ambapo ametoa wito kwa Mikoa,wilaya,kata na Matawi kuhakikisha Ajenda ya kuongeza wanachama wapya wa makundi mbalimbali inakuwa ni Ajenda ya kudumu.
Umoja wa wanawake Tanzania UWT umesema Kwa kutambua kuwa Wanawake ndio nguzo ya familia, itatimiza wajibu wake katika malezi, makuzi, ustawi na maendeleo ya watoto na familia ikiwemo kuhakikisha wanadumisha maadili, desturi na tamadumi chanya kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
No comments:
Post a Comment