DKT.MPANGO AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUINGIA KATIKA MAPAMBANO YA KUZUIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA - OKULY BLOG

Breaking

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA | PIGA 0785 364 965

Thursday, January 12, 2023

DKT.MPANGO AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUINGIA KATIKA MAPAMBANO YA KUZUIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na Viongozi, Wananchi pamoja na Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akipata akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Joseph Mafuru kabla ya kuanza kupanda miti katika Shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12, 2023.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda ,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Katibu Mkuu wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Pili Mbanga,akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango kuongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akipanda mti aina ya Mdodoma kandokando ya barabara ya Dodoma – Morogoro eneo la Ihumwa Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akipanda mti aina ya Msabuni katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akimshuhudia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo wakati akipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akimshuhudia Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda wakati akipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akimshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule wakati akipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akimshuhudia Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde wakati akipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akimshuhudia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa wakati akipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akiwashuhudia Wakuu wa wilaya Mkoa wa Dodoma wakati wakipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akiwashuhudia Mabalozi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma wakati wakipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akiwashuhudia Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msalato wakati wakipanda mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akishuhudia baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na vyuo vilivyopo mkoani Dodoma wakipanda mti aina kandokando ya barabara ya Dodoma – Morogoro eneo la Ihumwa Jijini Dodoma wakati alipoongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule za msingi Ihumwa mara baada ya kumaliza zozezi la upandaji miti kandokando ya barabara ya Dodoma – Morogoro eneo la Ihumwa Jijini Dodoma wakati alipoongoza zoezi la upandaji miti hiyo kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi mara baada ya kuongoza zoezi la upandaji Mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari mara baada ya kuongoza zoezi la upandaji Mti katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo Januari 12,2023.

Na Okuly Julius-Dodoma

MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango, amewataka Waandishi wa Habari kuhakikisha wanakuwa mabalozi wema wa kutangaza umuhimu wa upandaji miti na utunzaji wa mazingira pamoja na kuingia katika mapambano ya kuzuia uharibifu wa hifadhi ya misitu kwa kutumia kalamu zao.

Dk. Mpango ameyasema hayo leo Januari 12,2023 Jijini Dodoma, wakati wa kilele cha upandaji miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibari.


“Waandishi wa habari mnayo kazi kubwa ya kutumia vifaa vyenu kupaza sauti juu ya umuhimu wa upandaji miti na utunzaji wa mazingira kwa ujumla wake sambamba na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na miti mingi ”amelezea Dk.Mpango.


Pia Dkt.Mpango ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinapanda miti milioni 1.5 kwa lengo la kuhamashisha utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko tabianchi kama ilivyoelezwa katika ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi.

"Natamani kuona miti milioni 1.5 katika kila Halmashauri zikiwa zimepandwa na kukua kwa sababu hayo ndio maelekezo yaliyopo katika Ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi lengo ni kuifanya Tanzania kuwa ya kijani,"amesema Dkt.Mpango

Akihitimisha kilele hicho katika shule ya msingi ya Msalato Jijini Dodoma, Dk.Mpango amesema Tanzania inatakiwa kuwa nchi ya kijani na kila mtu anao wajibu wa kupanda miti katika eneo lake la makazi au katika taasisi.

Sanjari na hiyo, Dkt.Mpango amezitaka taasisi zote kujenga utamaduni wa kuhakikisha zinapanda miti katika maeneo yao ili kuondokana na janga la ukame.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema tayari mipango mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira imeanza kutekelezwa ikiwemo kugawa maeneo yaliopandwa miti kwa taasisi za serikali na binafsi ili waweze kusimamia na kuhakikisha miti hiyo inaishi.

Waziri Jafo amemuhakikishia Makamu wa Rais zoezi la upandaji miti na kuitunza miti hiyo litakua endelevu wakati wote.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, amewataka wataalamu wa misitu kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii namna sahihi ya kupanda miti.

“Tunaposema kuwa tunahitaji kupanda miti ni lazima tutambue kuwa tunahitaji kupanda miti gani,wapi na wakati gani.

Na kuongeza kuwa “Je tunaposema tupande miti tunapanda miti kwa kutumia nini ,tunatakiwa kutambua kuwa tunatakiwa kuchimba shimo kubwa la futi tatu kwa kinana upana wa futi tatu na tutumie udongo wa juu kwa kuchanganya na mbolea ya samamdi ili kupanda mti kwa kuzingatia kumwagilia na kushindilia vyema udongo”ameeleza Pinda.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alimweleza Makamu wa Rais Dk. Mpango kuwa nia ya jiji ni kuhakikisha inapanda miti katika maeneo mbalimbali zikiwemo shule za msingi na sekondari.

Mafuru ameeleza kuwa katika utekelezaji wa zoezi la upandaji miti tayari wamepanda miti ya aina mbalimbali katika shule mpya ya msalato miti 1,000 kwenye eneo lenye ukubwa wa hekari 6.2.

No comments:

Post a Comment

HABARI KUU KWA SASA

HABARI ZILIZOPEWA UZITO WA JUU KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 17,2024